MWONGOZO WA SUALA LA KUTAFSIRI NCHINI TANZANIA A. S. NCHIMBI* 1. Kwa watu wengi, neno hili la TAFSIRI ni la kawaida katika mazungurnzo yao ya kila siku. Maana inayoeleweka na kukubalika na wengi wetu ya neno hili TAFSIRI-ni ile ya kutoa "maana" ya hahari fulani "Maana" hiyo inaweza ama kutolewa katika maneno ya lugha ile ile (L1) ya habari ambayo inatarajiwa kutafsiriwa: (t=m+a),l ama katika lugha tofauti (~) na ile (L1) ya habari yenyewe inayotarajiwa kutafsiriwa: (t-;"~ml+al)' Wana-Isimu wa siku hizi wamekubaIiana kwamba hapana uwezekano wa "kuitafsiri habari fulani" iIiyoandikwa katika lugha L1 katika lugha K2 kwa asilimia 'mia moja taslim.' Maadam TAFSIRI inamhitaji anayetafsiri kufa- hamu barabara habari yenyewe inayotarajiwa kutafsiriwa, yaani Ll na pia kuifahamu barabara miundo mbaIi mbaIi ya lugha ~ ambamo TAFSIRI hiyo itafanyika, ni dhahiri kwamba aina yo yote ya TAFSIRllazima ifanyike katika lugha ambayo anayetafsiri awe amezaliwa nayo. Zaidi ya hayo, mambo ambayo yanasaidia kuifanya TAFSIRI yo yote iwe sahihi zaidi ni elimu ya mfasiri katika utamaduni, siasa na mazingira ya nehi ambamo lugha zinazotu- mika katika TAFSIRI hiyo zimekomazwa.8 2. Kwa nini TAFSIRI ni muhimu katika maisha yetu ya kila siku? SwaIi hili ni muhimu sana, kwani tusipofafanua umaarufu wa T AFSIRI katika maisha yetu ya kila siku, basi ni halali pia kusahau suala la TAFSIRI. Lakini ukweli ni kwamba maisha yetu daima hujitafsiri kufuatana na utamaduni wetu, siasa yetu na mazingira yetu. Kwa hiyo, suala la TAFSIRI ni la faradhi katika maisha ya binadamu. Kwa mfano, ni sisi Watanzania pekee tunaoweza kuhisi jinsi gani siasa ya Ujamaa na Kujitegemea inavyoweza kutusukuma mbele kwa haraka kimaendeleo kutokana na utamaduni wetu, ujuzi wetu wa siasa zingine mbaIi mbali, na mazingira ya nehi yetu yaIivyo. Kutokana na hisi zetu katika mambo hayo mbaIi mbali ambayo yanafanya sehemu muhimu ya ubinadamu wetu, ndipo tutakapoweza kutoa TAFSIRI iliyo sahihi kabisa; kwani lugha pekee ndiyo inayoweza kueleza bisi hizo katika mambo hayo mbaIi mbaIi. Kwa biyo, ni dhahiri kwamba mfasiri anayetumia lugha mbili ambazo kwake yeye ni za kigeni tupu, aghaIabu hutoa TAFSIRI zilizo sahibi. 3. Ni matumaini yetu kwamba cho chote wanachofanya Watanzania hapa makwao au katika ncbi za ng'ambo, lazima kiwe kwa manufaa ya Watanzania wenyewe; na hasa kwa manufaa ya wale waisbio nyumbani, Tanzania. Ni tegemeo letu pia kwamba wafanyakazi wa kigeni hapa ncbini katika kutekeleza •A. S. Nichimbi is an assistant lecturer in the Department of Languages and Linguistics, 99 University of Oar es Salaam. wajibu wa kazi zao, lazima uwe katika kulifikia lengo hilo hilo, yaani "kwa UTAFlTI ajili ya manufaa ya Watanzania wenyewe." 4. Lugha itumiwayo na Watanzania wengi hapa nehini katika utatuzi wa vikwazo mbali mbali vinavyowakabili katika maisha yao ya kila siku ni KISW A- HILI ambacho msamiati wake ni mchanganyiko wa maneno mbali mbali ya vijilugha vyote vya hapa nchini vyenye asili ya Kibantu. Zaidi ya hapo, kuna maneno mengine pia yaliyojiingiza katika KISW AHILI yenye asili ya lugha za Watawala wetu wa Kikoloni; kama vile maneno yenye asili ya Kiarabu, Kireno, Kifaransa, Kijerumani, Kiingereza, n.k. Sarufi ya Kiswahili ni ya kibantu kitupu. Kwa Watanzania, KISWAHILI ni lugha yao ya Taifa tangu mwaka 1968. Ingawaje uamuzi huu ulichelewa kutamkwa rasmi na serikaIi, ukweli ni kwamba, kwa muda wa kame nyingi, KISW AHILI kimejidhihirisha kwa Watanzania wengi, kwamba ndiyo lugha pekee ambayo wameitumia katika mawasiliano tangu enzi hizo mpaka leo katika maisha yao ya kila siku. 5. Tangu mwanzo wa kame hii ya ishirini, Watanzania tumeonyesha ari ya kutaka kujifunza lugha za kigeni; sio zile tu za waliokuwa Watawala wetu wa Kikoloni, kama vile Kiarabu, Kijerumani na Kiingereza, bali pia Kifaransa, Kireno, Kirusi, na nyingi nyinginezo. Kwa hivi sasa, lugha rasmi za kigeni ambazo Watanzania tunajifunza kusema na kuandika kwa ufasaha ni Kiinge- reza na Kifaransa;nazo hufundishwa katika mashule yetu ya hapa nehini kwa idhini ya serikaIi ya Wananchi wenyewe. Si ajabu kwamba serikali ya Wananchi huenda ikaamua kuongeza ufundishaji wa lugha zingine za kigeni katika mashule yetu hapa nchini hapo baadaye, kama vile Kireno, Kichina, Kijerumani n.k. 6. Mara nyingi, Watanzania wanapoamua jambo fulani kwa njia ya serikaIi yao huwa wana sababu mahsusi. Sababu ya uamuzi wa serikali ya Tanzania wa kukifanya Kiswahili kuwa Lugha ya Taifa ni kwamba lugha hii, kama ilivyosemwa hapo awali, ni lugha ya mawasiliano baina ya Watanzania; zaidi ya hayo, KiswahiIi ni sehemu muhimu ya utu wa Mtanzania kwani ndiyo lugha pekee anayoweza kuitumia kueleza kinaganaga utamaduni wake, siasa yake na mazingira ya nehi yake huyo Mtanzania. Hivi leo, Kiswahili kinatumika katika kufundishia masomo mbali mbali ya Pani na Sayansi katika shule nyingi na vyuo vingi nehini. Kiingereza na Kifaransa hufundishwa kama lugha za kigeni hapa nchini. Moja wapo ya sababu muhimu zilizopendekezwa na wananchi katika kuamua ufundishaji wa lugha mbili hizi za kigeni hapa nehini, ni kwamba lugha mbili hizi hutumiwa na watu wengi hapa duniani ambao kimaisha wanatuhusu sana; kwa mfano, tunaendelea kujifunza Kiingereza kwa sababu Waingereza bado tunahusiana nao. Tunajifunza Kifaransa kwa sababu kuna Waafrika watumiao lugha ya Kifaransa na ambao tunahusiana nao sio katika Uafrika tu, bali pia katika uendeshaji wa vita vyetu vya kulikomboa bara letu la Afrika kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Kiwe Kiswahili au Kiingereza, Kifaransa au Kireno, n.k. tunajifunza lugha hizi ill pawepo na mawasiliano ya hall ya juu baina yetu sisi Waswahili na hao wenzetu watumiao lugha zingine wakati tunapokabitiwa 100 UTAFITI na tatizo Iinalotuhusu wote katika jumuia yetu. Mataifa ambayo huhusiana katika usawa wa matatizo yao lakini ambayo yanatofautiana katika lugha, hayana budi kuanzisha madarasa ya kuwafundisha wananchi wake lugha zinazowahusu. Kwa mfano, iwapo sisi Watanzania tuna uhusiano wa aina fulani na Wachina, uhusiano ambao utasababisha pande zote mbili hizi kuonana mara kwa mara katika jitihada zetu za kutatua tatizo fulani linalotukabili, basi hapana budi serikali ya Watanzania iamue kuanzisha madarasa ya kuru- ndishia wananchi wake lugha ya KICHINA. Hali kadhalika, serikali ya Wachina itabidi iamue kuanzisha madarasa ya kufundishia wananchi wake lugha ya Watanzaoia, yaani KISWAHILI. Iwapo nadharia kama hii ingedhihirishwa kimatendo tangu miaka mingi iliyopita kati yetu sisi Watanzania na Wachina, TAFSIRI ambayo ingetumika wakati wa mikutano mbali mbali ya Wakuu wa serikali za mataifa hayo mawili katika jitihada zao za kutafuta jawabu la suala linalowakabili ingekuwa imechukua sura kama ifuatayo: l. Kwa upande wa Wachina: KISW AHIL! ) KICHINA (Lugha ya kigeni) (Lugha ya kwao) (Mchina aliye hodari katika Kiswahili na aliyefuzu utaalamu wa kutafsiri atahitajika kumtafsiria katika Kichina Mkuu wa serikali yake yale yase- mwayo kwa Kiswahili na Mkuu wa serikali ya Watanzania katika mku- tano huo). II. Kwa upande wa Watanzania: KICHINA--- -.--------.-~KISW AHIL! (Lugha ya kigeni) (Lugha ya kwetu) (Mtanzania aliye hodari katika Kichina na aliyefuzu utaalamu wa kutafsiri atahitajika kumtafsiria katika Kiswahili Mkuu wa serikali yetu yale yasemwayo kwa Kichina na Mkuu wa serikali ya Wachina katika mkutano huo). 7. Ni dhahiri kwamba kama pangekuwa na haja, Mwalimu-Mtaalamu wa Kichina wa kutafsiri Kiswahili katika Kichina angeweza kuajiriwa na serikali ya Watanzania ili nasi pia tuupate utaalamu wa kuitoa tafsiri iliyo sahihi zaidi yenye sura kama ifuatavyo: Ill. KISW AHIL! ) KICHINA (Lugha ya kwetu) (Lugha ya kigeni) Hali kadhalika, Mwalimu Mtaalamu wa Kitanzania wa kutafsiri Kichina katika Kiswahili angeweza kuajiriwa na serikali ya Wachina ili nao pia wapate utaalamu wa kuitoa tafsiri iliyo sahibi zaidi yenye sura kama ifuatavyo: IV. KICHINA+-- --+KISWAHIL! (Lugha ya kwao) (Lugha ya kwetu) Ndiyo kusema kwamba katika nchi bizi mbili tuogeshuhudia kuwepo kwa madarasa yanayofundisha wanaochi wake tafsiri zenye sura mbili, kama zifuatazo: (a) K wa sisi Wataozania, sura za TAFSIRI zetu ziogekuwa kamazifuatazo: 101 V. KICHINA+-- --+KlSWAHIL! UTAFITI j- ~ .- i - -- S , , r. ! ~ - .~ Q c ~ - c t- >.. -- ~ ~ 0 >.. .I! J! :;2 , ~ ...,.c >.. ~- Q , ii .. J! .c ;; >.. , t- ..J ~ ~ j. UTAFITI (b) Kwa wenzetu Waehina, sura za TAFSIRI zao zingekuwa kama zifua- zo: VI. KISWAHILI~ ~KICHINA 8. Ni lazima ikumbukwe daima kwamba MTU BINAFSI ana namna yake pekee ya kufafanua jambo fulani katika jitihada yake ya kulitafsiri jambo hilo kwa uwezo wake wote; TAIF A nalo pia, lina msimamo wake katika ufafanuzi wa jambo fulani ili kulitafsiri jambo hilo kwa usahihi wa hali ya juu liwezavyo; JUMillA NDOGO YA MATAIFA HURU, nayo pia, ina msimamo wake mahsusi ambao huenda ukawa tofauti na ule wa MTU BINAFSI au wa TAIFA fulani katika ufafanuzi wa jambo fulani iIi kulitafsiri jambo hilo kwa usahihi wa hali ya juu iwezavyo. IIi pawepo na uwezekano wa kufafanua jambo fulani katika jitihada ya kulitafsiri jambo hilo kwa usahihi "a hali ya juu iwezeka- navyo, anayehusika na ufafanuzi huo wa hali ya juu na hatimaye kuifikia tafsiri i/iyo sahihi kabisa, hana budi kutumia ujuzi wake wote wa (i) utamaduni wa Taifa lake, (ii) siasa ya Taifa lake, na (iii) mazingira ya nehi yake yote. Kwa hiyo, katika kupeana mawazo juu ya tatizo fulani linalokabili MAT AIF A mawili ambayo yamepania kumaliza tatizo hilo, lazima kila TAIF A, kwa upande wake, litumie lugha ya Wananchi wake katika kujieleza bila wasi wasi kifikra kuliko kuwa katika hali ya juu. Twaweza kufafanua zaidi haya yaliyo- semwa hapo juu. Twaweza kufafanua zaidi hayo yaliyosemwa juu kwa msaada wa mehoro ufuatao: 9. Mabwana zetu Waingereza (na hata baadhi ya Watanzania wenzetu waliolewa kasumba ya kusema na kuandika lugha ya Kiingereza) wangependa kuona kwamba habari zinazosemwa au zilizoandikwa katika lugha zingine zote zitafsiriwe katika lugha ya Mabwana zetu Waingereza-yaani Kiingereza. Kwa hiyo, sura za utumiaji wa lugha mbali mbali katika Tanzania wangependa ziwe kama zifuatazo: (i) Katika mawasiliano ya aina yo yote kati ya Watanzania wenyewe kwa wenyewe, sura ya utumiaji wa lugha ingekuwa kama ifuatayo: Kiswahili-----------------+Kiingereza au Kiingereza~ ~ Kiingereza (ii) Katika mawasiliano kati ya Watanzania na watu wa mataifa mengine, sura ya utumiaji wa lugha mbali mbali katika Tanzania ingekuwa kama ifuatayo: Kireno Kihispaniola Kijerumani Kiingereza Kifaransa Kiarabu 103 --~--- \ \ \ N " N \ .!! ;;. N N " \ N ~" ~ ~ ;;2~ :i -0 i: 1 ,----- :=1 " :"1 ~, i \ "" \ I - -- \ 1- I \ / / / / ~ I.... / = g ..~ .... " ~ -- UTAFITl n.k. Jibu linalotoka kwa Watanzania kwenda kwa mataifa hayo wangependa liwe kwa Kiingereza. Lakini tukiehunguza sana mpango huu wa matumizi ya lugha hizi, tutaona kwamba kuna mushkeli mahali fulani. Kwa mfano: (a) Ni dhahiri kwamba Watanzania hawajui Kifaransa, lakini Waingereza wengi wanajua Kifaransa. Iwapo tatizo lilikuwa linawahusu Watanzania na Wafaransa, basi Taifa la Tanzania lingelazimika kuajiri Wataalamu wa Kiingereza wa kutafsiri Kifaransa katika Kiingereza. Na iwapo tatizo hilo lingekuwa Ia kudumu, basi haja ya kuwaajiri Wataa- lamu-Waingereza ingekuwa ya kudumu pia. Ni dhahiri kwamba, hii ni njia mojawapo ya sisi wanyonge kujiona tunalazimika kumpa kazi Mwingereza. Na Waingereza, kwa upande wao, wangeweza kutumia mbinu kadha wa kadha ili kuudumisha unyonge wetu huo wa kujiona kwamba tunalazimika kumuajiri kila mara yeye tu katika kazi za aina hii. Kwa hiyo iwapo Watanzania walio wengi wangependa kuarifiwa mambo yaliyozungumzwa kati ya Wakuu wa serikali ya Wafaransa na Wakuu wa serikali yetu, Wakuu wa serikali yetu ingewabidi wapate TAFSIRI ya habari iliyoandikwa au iliyosemwa kwa Kifaransa katika Kiingereza kwanza, halafu apatikane Mtaalamu mwingine wa kutafsiri tafsiri hii ya Kiingereza katika Kiswahili, lugha ambayo sasa itumike kuwaarifu Watanzania wote kwa njia ya magazeti na taarifa za habari za Idhaa ya Redio, Tanzania. Twaweza kuionyesha sura ya mfano huu wa matumizi ya Iugha hapa Tanzania kama hii ifuatayo: (b) Mwanaehuo Mtanzania wa Chuo Kikuu eha Dar es Salaam anayeamua kuehukua tafsiri inayohusu lugha za Kiingereza na Kifaransa-{Kiingereza ~Kifaransa) yu katika mkondo wa kuzishughulikia lugha mbili zilizo ngeni kwake kwa kila hali. KITA MA DUNI hapana Jugha hata moja kati ya hizo mbili inayoweza kueleza kinaganaga hisi zetu; KIJIOGRAFIA, Iugha zote mbili hizi zimetoka mbali sana na Tanzania-yaani, Uingereza na Ufaransa. Kwa hiyo, mazingira ambamo lugha mbili hizi zimekomaa ni mageni pia kwa Mwanaehuo-Mtanzania. Mtindo wa SIASA ya Wai- ngereza na Wafaransa ni tofauti na huu wetu sisi Watanzania: Kiingereza na Kifaransa ni Iugha zilizokomazwa, na zinaendeIea kukomazwa zaidi, katika SIASA ya kibepari. Mwanaehuo-Mtanzania anakomazwa katika SIASA ya Ujamaa na Kujitegemea iliyofanana sana na mila za kabila lake. Lakini kwa upande mwingine, tafsiri hii hii inayohusu Iugha za Kiingereza na Kifaransa-(Kiingereza+- ---+Kifaransa) si ngeni kwa hali yo yote kwa Mwanaehuo-Mwingereza au Mwanaehuo-Mfaransa kwa sababu ambazo ni dhahiri. Kwa hiyo, ukweli ni kwamba Mwanaehuo-Mtanzania wa Chuo Kikuu eha Dar es Salaam anapotahiniwa juu ya tafsiri ya habari inayohusu lugha ya Kiingereza na Kifaransa, itambidi ajitahidi mara dufu zaidi kuIiko Mwanaehuo-Mwingereza za wa Chuo Kikuu eha Landani au 105 Mwanachuo-Mfaransa wa Chuo Kikuu eha Parisi kama nao hao wange tahimiwa juu ya tafsiri ya habari hiyo ili matokeo yao ya mwisho, baada ya UTAFm masahihisho ya mitihani yao, yastahili, kama alama ya asili-mia arobaini (40%). Kwa Mwanachuo-Mwingereza au Mwanachuo-Mfaransa, tafsiri ya aina hii, yaani-Kiingereza~ -Kifaransa, ni ya kawaida kwake; kwani lugha mojawapo ya hizo mbili, kwake ni ya kuzaliwa nayo. Kwa hiyo, alikuwa amefanya mtihani wa kutafsiri lugha ya kigeni katika lugha ya kwake. Na apewapo alama ya asili-mia arobaini (40%) kwa kazi yake, walimwengu wake watamweka mahali pake katika kusifiwa; yaani, kama ni HODARI au HODARI WA WASTANI au HAFA! kwa kutafsiri. Kwa kawaida ya Vyuo Vikuu mbali mbali vya ulimwengu, alama ya asili-mia arobaini (4O%=C) inastahili sifa hii: HODARI WA WASTANI. Mwanachuo- Mtanzania aliyepata alama ya asili-mia arobaini (40 %), atawekwa mahali gani kisifa na walimwengu wake? Akumbuke kwamba mtahiniwa huyu ilimbidi ajifunze kwanza lugha mbili hizi, yaani Kiingereza na Kifaransa, kabla ya kujifunza isimu yake na hatimaye kuitumia elimu hiyo katika majaribio ya kiutalaamu, kama mitihani hii ya kutafsiri. Mtahiniwa mwenzake Mwanachuo-Mwingereza au Mwanachuo-Mfaransa hakuwa na haja ya kujifunza kwanza lugha yake hapo chuoni pake kwa sababu lugha hiyo amezaliwa nayo; yeye alianza kujifunza moja kwa moja isimu ya lugha yake na utaalamu wa kuitafsiri lugha yake katika lugha ya kigeni kwa muda wake wote alioishi hapo ehuoni pake. Mara nyingi Vyuo Vikuu mbali mbali vya ulimwengu vimetumia wembe ule ule-yaani a1ama ya asili-mia arobaini (4O%=C) istahili sifa ya: HODARI WA WASTANI, Uamuzi huu ni sawa: lakini matokeo yake ni mabaya kwa upande wa Mwanachuo-Mtanzania. Ukweli ni kwamba kwa Mwanachuo-Mtanzania anayestahili alama ya asili-mia arobaini (4O%=C) ana aki/i zaidi kuliko Mwanachuo-Mwingereza au Mwana- ehuo-Mfaransa anayestahili alama ya asili-mia arobaini (40%=C) katika mtihani huo wa kutafsiri Kiingereza~Kifaransa. Yaani, Mwanaehuo- Mtanzania aliyestahili kupata alama ya asili-mia arobaini (40 % =C) ingebidi alingane na Mwanachuo-Mwingereza au Mwanaehuo-Mfaransa aliyestahili kupata a1ama ya asili-mia, kama hamsini na tanG (55%=B). Hii ina maana kwambajuhudi ambazo tungetegemea Mwaoaehuo-Mtanzania (40%) kuzionye- sha katika utekelezaji wa wajibu wake wa kazi za Wizara au Shirika lililomwajiri ingeliogana na i1ejuhudiya Mwanachuo-Mwingereza au Mwanachuo-Mfaransa (55%). Lakini kwa sababu ya unyonge wetu, tunalazimika kumtukuza Mwanaehuo- Mwingereza (4O%=C) au Mwanachuo-Mfaransa (4O%=C) kwa kumtunukia sifa ya Mwanachuo-Mtanzania wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayestahili sifa ya a1ama ya asili-mia (55 % =), yaani, HODARI. Unyonge huu wa TAIF A la Watanzania kujiona kwamba wanalazimika kumwajiri Mwingereza, eti kwa sababu ya ujuzi wa lugha yake ya Kiingereza na nyinginezo za huko Ulaya, kutufanyia kazi ya kutafsiri habari yo yote itokapo papa hapa nchini au nehi za nje, waweza kupigwa vita, na. unyonp 106 UTAFITI wetu huo kutoweka kabisa katika TAIFA letu, iwapo tu, tukikubaliana kushiri- kiana katika utekelezaji wa mambo haya yafuatayo: I. Sisi Watanzania tukatae kuamini kwamba ni lugha ya Kiingereza tu inayoweza kueleza utamaduni, siasa na mazingira ya binadamu kote ulimwenguni na kwamba lugha zingine, lugha yetu tukufu ya Kiswahili ikiwa mojawapo haziwezi kufanya hivyo. II. Sisi Watanzania tujenge imani kwamba lugha yo yote ya binadamu katika taifa lake imejikamilisha yenyewe katika kueleza vilivyo utamaduni, siasa na mazingira ya binadamu wa taifa hilo kuliko lugha nyingine yo yote ya bandia. III. TANU na vyombo vyake, vizidi kutoa uamuzi wa busara wa kimapinduzi katika jitihada yake ya kukomboa wananchi wake. Kwa mfano, izidi kutoa uamuzi wa kutumia lugha ya Kiswahili katika ufundishaji wa masomo yote ya shule za hapa nchini, kufuatana na hali ilivyo katika shule hizo. IV. Sisi Watanzania tusiwe chanzo cha kuwepo kwa hali ambayo inaweza kusababisha uzorotaji katika kutekeleza jambo Namba III hapo juu. IIi uepukane na sifa mbaya kama hii, itakubidi, na hasa ukiwa kama Kiongozi wa wenzako hapo kazini au hapo uishipo, kuwahoji wenzako juu ya njia mbali mbali ambazo zingesaidia kutatua vikwazo vya hapo kazini au kijijini penu. V. Sisi Watanzania tuwe macho kugundua hila zo zote za wageni za kutaka kuunyonya utaalamu wetu katika utamaduni wetu, siasa na mazingira yetu. VI. Kutokana na yale tunayoyashuhudia yanatokea mwaka hata mwaka katika taifa letu; sisi Watanzania tunaamini kwamba taifa letu linaendelea. Tunaposema kwamba taifa linaendelea, tunamaanisha kwamba binadamu wa taifa hili wanaendelea; na kuendelea kwa binadamu ni kuendelea kwa utamaduni wake, siasa yake na mazingira yake pamoja. Lugha pekee ya binadamu wa taifa 10 lote ndiyo itakayoweza kueleza maendeleo hayo katika daraja mbali mbali zilizotajwa hapo juu. Kwa sisi Watanzania, lugha iliyo na jukumu kama hili ni Kiswahili. VII. Sisi Watanzania, tujenge moyo wa kutafutatafuta msamiati wa kitaalamu katika mambo mbali mbali yanayotuhusu. Tufundishane msamiati huo ili tuutumie vilivyo katika mawasiliano yanayotuhusu. 10. Kwa kuwa KlSWAHILI ndiyo lugha ya Taifa la Watanzania wanaoende- lea mwaka hata mwaka kiutamaduni, kisiasa na kimazingira, ninapenda sura za matumizi ya lugha hapa nchini ziwe kama zifuatazo: (i) Katika mawasiliano kati ya Watanzania wenyewe kwa wenyewe: Kiswahili +- -Kiswahili. (ii) Katika mawasiliano kati ya Taifa]a Watanzania na Mataifa mengine: Hapana budi tukumbuke pia, kwamba iwapo Watanzania tutatilia mkazo 107 zaidi katika TAFSIRI zinazohusu KISWAHILI na lugha yo yote yenye asili UTAFITI Lugha ya Kigeni -=======================--,:,-,:,-,:,-,:,-':'-+_,Kiswahili +- Kwa mfano: (a) Kikemba +- ______________ -+_Kiswahili (b) Kiingereza +- ______________ -_Kiswahili (c) Kiarabu ______________ -+._Kiswahili +- (d) Kilingala ______________ -+_Kiswahili +- (e) Kifaransa +- ______________ -+_Kiswahili (f) Kiwolofu _____________ -+_Kiswahili +- (g) Kiurdu _____________ -+_,Kiswahili +- (h) Kihausa +- _____________ -+_Kiswahili (i) Kireno +- _____________ -+_Kiswahili U) Kichina +- ___________ .__ -'>_Kiswahili ya Mwafrika, tutakuwa tunauendeleza sio utaalamu wetu katika kutafsiri tu, bali pia utamaduni wa Mwafrika, siasa ya Mwafrika, mazingira ya Mwafrika na hasa lugha ya Mwafrika. FOOTNOTES I. ambapo: (t, m, a, )=L1 2. (t, m',a', )L=2 3. Kutokana na yaliyomo katika kitabu kiitwa.cho: "Language- Teaching Abstracts", Volume 7, No.3, July, 1974). 4. Neno hili Mabwana (wengi) Bwana (mmoja), linaonyesha kwamba kati ya wale wanaolitumia, mmoja wao ni mtwana. Siku hizi, Watanzania hutumia neno Ndugu. t08 SUMMARY THE RATIONALE OF TRANSLATION IN TANZANIA This article is purely the author's point of view with regard to the use of languages in the day~to-day official duties of a Tanzanian residing in his home country. Apart from Kiswahili, his national language, the Tanzanian official is faced with another problem: that of having to consult an expa- triate officer who does not know Kiswahili on matters of grea.t national in,terest. In this matter he has at least one alternaltive: the use of the English language. But Tanzania has invited so many expatriate officers to carry out different national projects. Not all of these expatriate officers are English- speaking; we have French, Germans, Scandinavians, Russians, Chinese, etc., who would like to express their feelings to Tanzanian nationals in their respectilVe native languages. Is ~t not true that the use of a native language by its native speaker is an indication of what this native speaker really intends to convey to the public concerned? On the other hand is it not true that the use of a native language by a non-native speaker may not be an indication of what this non-native speaker really wants to convey to his public? The non-English expatriate officers and surely the Tanzanian nationals themselves, may be victims of this second category. Every time Tanzanians have expressed their feelings about a certain problem by using the English language to English nationals, we have never been fully understood by the na,tive English speakers. As a result, the necessary and immediate action that ought to have been taken thereafter as required by the Tanzanian nationals is often delayed for years! The point has to be clarified again and again for the simple reason that the former wasn't clear enough! This article suggests only one of the possible ways by which Tanzania and her friends can overcomethio; crucial problem of being misunderstood by one or the other; the adoption of the "Rationa:1e of Translation in Tan- zania". This is based on the assumption that if two friendly nations speak different native languages, it is the duty of both nations to learn the native language of the other, so that in times of common crisis, what one nation says about it in its native language is clearly understood by the other friendly nation. This means getting down to translation work by both the nations concerned. As stated earlier, the national language of Tanzania is Kiswahili. The "Rationale of Translation in Tanzania" should, therefore, be from a foreign language into Kiswahili and vice versa, for instance: English ~ Kiswahili 109 French~Kiswahili; Chinese ~Kiswahili; Wolo~Kiswahili Hausa~Kiswahili etc. This type of translation should be encouraged in all our learning institu- UTAFITI tions including our places of work. It would automatically mean implement- ing the TAND and Government decision on the use of Kiswahili in the country which was pronounced in 1968. The type of translation whereby two foreign languages are involved is not adViisable in Tanzania for the purpose of large-scale nationaJ. interests. It trains nationals to think and reason entirely in foreign languages about ma1lters of our own national cUl'ture. Not only is the information distorted and misunderstood when using these foreign languages to describe our own cmture. but also practicaJly not one natiooal of present Tanzania would take heed of the information stated in the foreign languages. "Ensemble il nous mut cultiver Ie jardin mnza.nien! Le Kiswahiii est it la fois un prestige et une identire des indigenes du pays." 1.10